Kimbunga Sandy ni fundisho la kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Ban

9 Novemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu madhara ya kimbunga Sandy kilichokumba maeneo ya Caribbean na pwani ya Mashariki ya Marekani mwishoni mwa mwezi uliopita na kusema kuwa mataifa yatumie kimbunga hicho kuwa fursa ya kuangalia upya mambo yanayochangia mabadiliko ya tabia nchi.

Pamoja na kuelezea kuhuzunishwa kwake na vifo, majeruhi na uharibifu uliotokea, Ban amesema kimbunga Sandy kimedhihirisha kuwepo kwa tabianchi isiyo ya kawaida na hivyo nchi zikubaliane kupunguza matumizi ya gesi ya ukaa inayoharibu mazingira.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Halikadhalika Ban amesema Umoja wa Mataifa ulitenga dola Milioni Tano kwa ajili ya Cuba na dola Milioni Nne kwa ajili ya Haiti kutokana na athari za kimbunga Sandy huku Jamaica ikitarajia kupatiwa msaada wa dharura kwa ajili ya afya na chakula pamoja na kujengewa uwezo wa kupunguza madhara yatokanayo na majanga ya asili.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter