Raia wengi wa Sri Lanka waliokwenda nje wana matatizo ya kiafya:IOM

9 Novemba 2012

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamianji IOM limefichua kile ilichokieleza kukithiri kwa vitendo korofi vilivyowaandama raia wa Sri Lank walioenda nchi za nje kwa ajili ya kusaka kazi.

Ripoti hiyo imesema kuwa kiasi kikubwa cha raia hao sasa wamepatwa na magonjw ambalimbali na wengine kupoteza maisha kwa kujinyonga na kufariki kwa kawaida.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandaliwa na kitendo maalumu cha IOM kinachofuatilia ustawi wa raia wanaokwenda nchi za ng’ambo, imeonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2010 zaidi ya watu 313 walifariki duniani, na kati ya vifo hivyo 18 vilitokana na kujinyonga na wengine walifariki kutokana na magonjwa baada ya kuteswa.

Ripoti hiyo imesema kuwa visa vya kuteswa kwa wafanyakazi wa Sri Lank viliripotiwa kwa wingi zaidi katika nchi za Magharibi mwa Asia ikiwemo Mashariki ya Kati.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter