Baraza la Usalama lashindwa kuridhia maazimio thabiti kuhusu Syria

8 Novemba 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuridhia maazimio thabiti kuhuusu Syria, kwa mujibu wa katiba ya Umoja huo inayolipa baraza mamlaka ya kusimamia amani na utulivu duniani.

Balozi wa Colombia katika Umoja wa Mataifa Néstor Osorio ametoa kauli hiyo wakati akitambulisha rasimu ya ripoti ya mwaka ya Baraza la Usalama itakayowasilishwa kwenye Baraza Kuu la Umoja huo.

Ameelezea kipindi cha kuanzia Agosti 2011 hadi Julai mwaka huu kinachozunguzwa ndani ya ripoti hiyo kuwa kilikuwa ni kipindi cha matatizo na chenye matukio.

"Kuhusu Syria, ghasia ndani ya nchi hiyo imefikia kiwango cha juu. Baraza limeridhia taarifa kadhaa pamoja na azimio namba 2042 na namba 2043, lakini yale yaliyomo hayatekelezwi. Katika kujaribu kuchukua uamuzi kwa mujibu wa sura ya Saba ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, baraza la usalama liligawanyika. Na katika fursa tatu zilizojitokeza, ya mwisho kabisa ni ya mwezi Julai mpango wetu wa kupitisha azimio kwa kuzingatia sura hiyo ya Saba lilishindikana.”

Balozi Osorio amesema umuhimu na wajibu wa Baraza la Usalama wa kulinda amani na ulinzi duniani unakuwa wa msingi zaidi kwa sasa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter