Mwelekeo wa kuleta amani Libya unatia moyo: Mitri

8 Novemba 2012

Serikali ya Libya pamoja na wananchi wake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wamepiga hatua kubwa kurejesha utulivu nchini humo licha ya changamoto zilizopo.

Hiyo ni kauli ya Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchiniLibya, Tarek Mitri aliyoitoa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wakati alipolihutubia kuhusu hali ilivyo nchini Libya kwa njia ya video kutoka nchini humo.

Katika ripoti yake Mitri ametaja matatizo yaliyokumba nchi hiyo ikiwemo mapigano katika maeneo ya Bani Walid, Shanti na Tripoli pamoja na shambulio dhidi ya ofisi ya ubalozi wa Marekani huko Benghazi

Bwana Mitri amesema tarehe 21 mwezi Septemba mwaka huu, wakazi 30,000 wa Benghazi walishiriki katika kile kilichoelezwa kuwa ni maandamano ya kuokoa Benghazi.

(SAUTI YA MITRI)

Halikadhalika Bwana Mitri amesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia Libya, kwa mwaka mzima uliopita umekuwa ukishirikiana na serikali ya Libya, taasisi za kiraia na jumuiya ya kimataifa kujenga demokrasia nchini humo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter