Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za ASEAN ziangalie upya rasimu ya azimio lake kuhusu haki za binadamu: Pillay

Nchi za ASEAN ziangalie upya rasimu ya azimio lake kuhusu haki za binadamu: Pillay

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay amesifu kongamano la Bali kama fursa muhimu ya kuendeleza utawala bora, utawala wa kisheria na haki za binadamu miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini- Mashariki mwa Asia, ASEAN huku akitaka viongozi wa nchi hizo kuweka muda zaidi kuandaa azimio la kikanda la haki za binadamu.

Pillay amesema hayo wakati huu ambapo kongamano hilo la Bali likiwa limeanza leo huko Indonesia na rasimu ya azimio la haki za binadamu la nchi za ASEAN inatarajiwa kupitishwa wakati wa mkutano utakaofanyika baadaye mwezi huu huko Phnom Pehn, Cambodia.

Taarifa zaidi na George Njogopa: