UNHCR yasaidia kusuluhisha matatizo ya ardhi kaskazini mwa Sri Lanka

7 Novemba 2012

Miaka mitatu tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka, changamoto mpya zimeibuka wakati watu wakiendelea kurejea nyumbani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limekuwa likishirikiana na viongozi wa kitaifa na wadau wengine ili kusaidia kuhakikisha wakimbizi hao wanarejea kwa njia endelevu kwa kuzishughulikia baadhi ya changamoto hizo, zikiwemo nyumba za makazi, ardhi na mali zao.

Vita hivyo vilivyodumu miaka 26, na ambavyo vilimalizika mwaka 2009, viliharibu huduma muhimu, makazi na miundo mbinu, na kusababisha mamia ya maelfu ya watu kutoroka makwao kaskazini na mashariki mwa Sri Lanka.

Walipokimbia hivyo, wengi wao walipoteza stakabadhi muhimu, vikiwemo vyeti vya umiliki wa ardhi. Waliporejea, wengi wao hawakuwa na uwezo wa kuonyesha umiliki wao, kwani serikali haikuwa na huduma nyingi za umma. George Njogopa na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)