Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na Pakistani waandaa tukio maalum kutetea elimu kwa mtoto wa kike

UNESCO na Pakistani waandaa tukio maalum kutetea elimu kwa mtoto wa kike

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova na Rais Asif Al Zardani wa Pakistani watakuwa wenyeji wa tukio mkutano maalum wa ngazi ya juu wa kutetea haki ya elimu kwa mtoto wa kike.

UNESCO imesema mkutano huo ukiwa na maudhui, Mtetee Malala, tetea hali mtoto wa kike kupata elimu, utafanyika mjini Paris Ufaransa, tarehe 10 mwezi ujao sambamba na siku ya haki za binadamu duniani na lengo ni kuchochea utashi wa kisiasa wa kuendeleza mikakati inayomwezesha mtoto wa kike kwenda shule.

Malala ni mtoto wa kike aliyepigwa risasi na kujeruhiwa tarehe Tisa mwezi uliopita nchini Paksitani na kikundi cha Talibani kutokana na ujasiri wake wa kujitokeza hadharani na kutetea elimu ya mtoto wa kike.

Marais, viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale ya kimataifa, watu mashuhuri, vyombo vya habari ni miongoni mwa makundi yanayotajrajiwa kushiriki mkutano huo.