Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanza kusambaza chakula kwenye jimbo la Rakhine, Myanmar

UM waanza kusambaza chakula kwenye jimbo la Rakhine, Myanmar

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limeanza kusambaza chakula kwa zaidi ya wakazi Elfu 27 wa vitongoji vilivyokumbwa na mgogoro wa kikabila kwenye jimbo la Rakhine nchini Myanmar mwezi uliopita.

Msemaji wa WFP Elisabeth Byrs amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa idadi hiyo ya wat wanaopatiwa msaada ambao wamepoteza makazi yao itaongezeka katika ya wiki hii na kufikia Elfu 35 na kadri inavyowezekana itakabidhi misaada hiyo moja kwa moja kwa wakimbizi walio kwenye kambi.

Hata hivyo Bi. Byrs kuna kitongoji kimoja kilichokumbwa na mgogoro ambacho hawajafikisha msaada na kuwa wanahitaji dola Milioni 11 kukidhi mahitaji la sivyo watasitisha msaada mwezi ujao.

(SAUTI YA Bi. Byrs)

“Tutasambaza chakula kwa zaidi ya watu Laki Moja waliopoteza makazi Rakhine kwa miezi Sita ijayo. Hivyo basi tunahitaji haraka dola milioni 11 kwa ajili ya mahitaji ya chakula cha watu hao. Hili ni ombi letu kwa wahisani ili kuahkishka chakula kinaweza kununuliwa na WFP na kinasambazwa kwa wakati. Bila mchango wa uhakika kutoka kwa wahisani, WFP italazimika kuanza kupunguza mgao wa misaada kwa watu hao waliopoteza makazi ifikapo Disemba.”

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa vurugu za Rakhine za wiki mbili zilizopita zimesababisha vifo vya watu zaidi ya watu 89 na wengine Elfu 35 kupoteza makazi huku nyumba 5,300 na majengo ya kuabudu yakiharibiwa.