Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taka ni tatizo linahatarisha usafi wa maji, hewa, chakula duniani na afya: UNEP

Taka ni tatizo linahatarisha usafi wa maji, hewa, chakula duniani na afya: UNEP

Takriban tani bilioni 1.3 za taka huzalishwa mijini kila mwaka, na kiwango hiki kinatarajiwa kuongezeka hadi tani bilioni 2.2 ifikapo mwaka 2025, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia. Kwa sababu hii, hatua za haraka zinahitajika ili kukabiliana na athari za tatizo hili kwa maisha ya mwanadamu, limesema Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP.

Tatizo hili linalozidi kukua ndilo limekuwa suala la kipaumbele miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano wa UNEP wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu udhibiti wa taka mjini Osaka, Japan. Mkutano huo umewashirikisha wataalam wa taka kutoka kote ulimwenguni, ili kutafuta suluhu kwa changamoto zinazohusiana na taka. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)