Uhuru wa kujieleza ndio kiungo muhimu cha kumaliza lugha za chuki:UM

6 Novemba 2012

Uhuru wa kujieleza unaweza kuchangia kuwepo kwa mazingira bora ya kuwepo kwa mazungumzo ya kukosoana hasa katika masuala ya kidini amesema mtalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza Frank La Rue.

Kupitia kwa ripoti yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjumbe huyo amezungumzia masuala ya lugha inayozua chuki na hatua za serikali dhidi ya suala hili. Mjumbe huyo amesema kuwa uhuru wa kujieleza unastahili kuondolewa ikiwa utazua hatari hasa ikiwa utatumiwa kuchochea watu kufanya mauaji ya halaiki au kuleta chuki.

Mtaalamu huyo alitaja jitihada za serikali nyingi za kuzuia matamshi ya kuzua chuki kama zilizokosa mwelekeo akiongeza kuwa sheria zinazotumika huwa zinalenga kuzima shutuma na kujieleza kisiasa. Amesema kuwa sheria zinazolenga kuzuia lugha za kuzua chuki zinahitaji kutumiwa kwa njia inayofaa ili kuzizuia kuingiali haki zingine za kujieleza.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter