Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahoji hatua ya serikali ya Sudan Kusini kumfukuza afisa wake wa haki za binadamu

UM wahoji hatua ya serikali ya Sudan Kusini kumfukuza afisa wake wa haki za binadamu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, Hilde Johnson, amesema hatua ya serikali ya Sudan Kusini kumfukuza afisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ni kinyume na wajibu wa serikali hiyo chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Kusini iliiandikia afisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS na kuamrisha afisa wake wa haki za binadamu aondoke nchini humo katika kipindi cha saa 48.

Bi Johnson amesema kuwa amekuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu zaidi nchini Sudan Kusini ili kupinga uamuzi huo wa serikali. Ameongeza kuwa ameiandikia serikali hiyo barua juma lililopita. Hata hivyo, amesema licha ya juhudi zote za ujumbe wa UNMISS, amri hiyo ya kumfurusha afisa wa Umoja wa Mataifa haijabadilishwa. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)