Tathmini ya mkataba wa kimataifa wa urithi wa dunia kufanyika Kyoto: UNESCO

5 Novemba 2012

Mkutano wa siku Tatu wa kuhitimisha kilele cha maadhimisho yaa miaka 40 ya mkataba wa kimataifa wa urithi wa dunia utafanyika mjini Kyoto Japan kuanzia kesho ambapo pamoja na mambo mengine utajumuisha mijadala kuhusu utekelezaji wa mkataba huo.

Tukio hilo linatarajiwa kushuhudia kuingizwa kwa eneo la 1000 la urithi wa dunia kwa mujibu wa mkataba huo uliopitishwa tarehe 16 November 1972 wakati wa mkutano mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, mkataba ambao unaelezwa kutambuliwa zaidi katika uhifadhi wa maeneo asilia na ya kitamaduni. Joshua Mmali na taarifa zaidi.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)