Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM yaongezewa wiki moja zaidi nchini Somalia

AMISOM yaongezewa wiki moja zaidi nchini Somalia

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza kwa siku saba zaidi muda wa kuwepo kwa vikosi vya kimataifa vinavyolinda amani nchiniSomalia.  Muda wa vikosi hivyo ulikuwa umalizike tarehe 31 mwezi uliopita.

Taarifa iliyotolewa imesema kuwa azimio la Barazahilolililopitishwa kwa kauli moja mjiniNew York, Marekani baada ya kikao chake, limeongezwa muda huo kwa kuzingatia mazingira ya kipekee yaliyokumba jiji laNew Yorkbaada ya kimbunga Sandy kilichoanzia hukoCaribbean.

Azimio hilo limetambua kuwa hali ya sasa nchini Somalia bado ni tishio la amani na utulivu kwenye eneo hilo la pembe ya Afrika na hivyo baraza limeamua kuongeza mamlaka ya ujumbe wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani Somalia, AMISOM na kuruhusu nchi za Afrika kuacha vikosi vyao hadi tareheSabamwezi huu.

Katika kipindi hicho vikosi hivyo vitaendelea kusaidia serikali yaSomaliakatika jitihada zake za kujenga amani na utulivu nchini humo.

AMISOM iliundwa mwezi Januari mwaka 2007 na Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika na kupata mamlaka yake ya utendaji kutoka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.