Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yakabiliwa na uhaba wa fedha kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

IOM yakabiliwa na uhaba wa fedha kuwasaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limeshindwa kuendesha juhudi za kuwakwamia mamia ya raia wa Pakistan waliokumbwa na mafuriko kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha.

Takwimu kutoka serikali zinasema kuwa kiasi cha watu milioni 3.4 wameathiriwa na mafuriko huku wengine zaidi ya 386,000 hawana makazi maalumu kutokana na nyumba zao kubomolewa na mafuriko hayo yaliyotokea miaka mitatu iliyopita.

Meneja wa IOM nchini Pakistan Izora Mutya Maskun amesema kuwa pamoja na kuhudi za shirika hilo kuwafikia wale walioathiriwa lakini mahitajio bado ni makubwa mno.

Amezihimiza nchi wahisani kuendelea kuchangia mafungu ya fedha ili kuwafikia mamia ya watu wanaoendelea kutabika bila ya huduma muhimu.