Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM waitaka Iran iwaachilie huru washindi wa Tuzo ya Sakharov mara moja

Wataalam wa UM waitaka Iran iwaachilie huru washindi wa Tuzo ya Sakharov mara moja

Jopo la wataalam huru wa Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa serikali ya Iran iwaachilie huru mara moja wakili maarufu wa kutetea haki za binadamu, Nasrin Sotoudeh na Jafar Panahi, ambaye ni mtengenezaji filamu mwenye umaarufu wa kimataifa.

Wawili hao walipewa tuzo ya uhuru wa dhana ya Sakharov hivi karibuni na bunge la Jumuiya ya Ulaya.

Wataalama hao huru wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Iran kutimiza wajibu wake wa kimataifa wa kulinda na kuendeleza haki za binadamu, hususan haki ya kujieleza na kuwa na dhana tofauti, na kuitaka imwachilie mara moja Bi Sotoudeh, Bwana Panahi na mawakili wengine watetezi wa haki za binadamau, ambao wamewekwa kizuizini kwa sababu ya kufurahia haki zao. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)