Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Umoja wa Mataifa mwaka huu wa 2012

Siku ya Umoja wa Mataifa mwaka huu wa 2012

Tarehe 24 mwezi Oktoba kila mwaka ni siku ya Umoja wa Mataifa, siku ya kusherehekea kuasisiwa kwa katiba ya kuanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945 baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Ikiwa ni miaka 67 tangu kuanzishwa kwake, Umoja wa Mataifa umepitia vipindi kadhaa vya raha na changamoto ambazo zimefanya Umoja huo kuimarika zaidi na zaidi. Katika makala haya Assumpta massoi atatuletea yaliyojiri katika maadhimisho haya hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, pamoja na maeneo mengine duniani.