Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani vikali shambulio wakati wa sala ya Eid el Adha huko Afghanistan

UNAMA yalaani vikali shambulio wakati wa sala ya Eid el Adha huko Afghanistan

Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya usaidizi nchini Afghanistan, UNAMA, imelaani vikali shambulio la leo kwenye msikiti mmoja huko Maimana katika jimbo la Faryab nchini humo lililosababisha vifo vya 4o na wengine 56 wamejeruhiwa.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchiniAfghanistan, Ján Kubiš, amesema shambuliohilolimetokea wakati wa sala ya Eid el Adha ambapo mtu aliyekuwa amevalia fulana yenye mabomu alijilipua wakati akiingia kwenye msikiti wa Eid Gah mjini humo.

Amesema shambuliohilobaya zaidi kwenye msikiti lililosababisha vifo vya raia waAfghanistanhalina uhalali wowote na linapaswa kushutumiwa na watu wote kwa nguvu zote.

Mwakilishi huyo amesema wahusika wanawajibika kwa vifo vilivyotokea kutokana na shambuliohilodhidi ya msikiti ambao kwa mujib uwa sheria za kimataifa za haki za binadamu haipaswi kushambuliwa kwa kuwa ni sehemu za ibada.

Kutokana na shambuliohiloUNAMA imetuma rambirambi zake kwa wafiwa na kuwatakia uponaji wa haraka majeruhiwa wote.