Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia kuhamisha waliokumbwa na kimbunga Haiti

IOM yasaidia kuhamisha waliokumbwa na kimbunga Haiti

Wakati kimbunga Sandy kikipita maeneo ya nchi za Caribbean na kusababisah vifo na mafuriko, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM nchini Haiti limechukua hatua za kinga usaidizi kwa kushirikiana na shirika la kiserikali la huduma za kibinadamu nchini humo DPC na lile la msalaba mwekundu nchini humo.

Hatua hizo kwa mujibu wa IOM ni pamoja na kusaidia kuhamisha watu zaidi ya Elfu Moja kutoka kambi zilizopo kwenye maeneo hatarishi kwenda makazi ya muda kwenye mji mkuu Port-au-Prince.

Halikadhalika vikundi vya kutoa msaada vilikuwepo katika kambi zote zilizohitaji msaada huku IOM ikisema kuwa kundi kubwa linalohitaji msaada zaidi wa hifadhi ni watoto na wanawake wanaoongoza familia zao wenyewe.

Kwa mujibu wa IOM kampeni za kuhamasisha watu kuondoka katika maeneo hatarishi zimefanyika katika kambi 176 ikiwemo 12 zilizo kwenye maeneo hatari ambapo asilimia 55 ya watu waliopoteza makazi yao wanapaswa kuhamishwa.

Makazi ya muda yana uwezo wa kuhifadhi watu Elfu Tano waliopoteza makazi yao.