Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia ni mahali pa kupendana na kumjali kila mtu: Stevie Wonder

Dunia ni mahali pa kupendana na kumjali kila mtu: Stevie Wonder

Mjumbe amani wa Umoja wa Mataifa Stevie Wonder amesema tangu akiwa mdogo alikuwa akifuatilia jinsi Umoja huo unavyojitahidi kuleta amani katika dunia na kusema kuwa alibaini dunia ni sehemu ambapo kila mtu anapaswa kumpenda na kumjali mwenzake kwa hali yoyote ile lakini baadhi ya watu wanaifanya pawe pahala pagumu pa kuishi.

Stevie Wonder ambaye anafahamika kwa utunzi wa nyimbo za amani na upendo amesema hayo alipozungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York baada ya kutumbuiza katika tamasha maaluum la kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA STEVIE WONDER)