Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za wanawake Bosnia- Herzegovina kumulikwa: Manjoo

Ukiukwaji wa haki za wanawake Bosnia- Herzegovina kumulikwa: Manjoo

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za wanawake Rashida Manjoo atakuwa na ziara ya siku nane nchini Bosnia Herzegovina kuanzia Jumapili yenye lengo la kukusanya taarifa kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za wanawake nchini humo.

Bi. Manjoo ambaye anawajibika kufuatilia vitendo vya ukiukwaji wa haki za wanawake, chanzo na madhara yake amesema ukiukwaji wa haki za wanawake umeenea zaidi duniani na kwamba vinakwamisha uwezo wa wanawake kufurahia uhuru wao na haki zao za msingi.

Wakati wa ziara hiyo, Mtaalamu huyo atakuwa na mazungumzo na watetezi wa kitaifa wa haki za wanawake nchini Bosnia Herzegovina kwa lengo la kupata picha halisi ya hali ilivyo nchini humo. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)