Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele na utapiamlo: WHO

Hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele na utapiamlo: WHO

Shirika la afya duniani, WHO limeomba washirika wake wa maendeleo na wale wa afya wazisaidie dawa nchi zilizokumbwa na njaa kutokana na mafuriko ambayo yanaweka mazingira ya mazalia ya vimelea vinavyosababisha magonjwa kama vile kichocho na trachoma au vikope.

Nchi zilizo hatarani zaidi ni zile za eneo la Sahel barani Afrika ambako pia migogoro ya ndani ya muda mrefu imesababisha uhaba wa chakula na hivyo hivyo kuweka hatari zaidi ya kuwepo kwa utapiamlo. WHO inasema kuwa mtu mwenye utapiamlo anakuwa hatarini zaidi kuambukizwa magonjwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)