Mkuu wa vikosi vya ulinzi wa amani UM ataka msukumo mpya kukabili changamoto za amani

23 Oktoba 2012

Mkuu wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa amejadilia kile alichokiita haja ya kubadili mkondo wa mambo pamoja na kuwa na majumuisho ya pamoja kwa duru za kimataifa ili kuzikabili changamoto za ulinzi wa amani ambazo zinakwaza operesheni mbalimbali duniani.

Amesema kuna haja ya jumuiya ya kimataifa kuwan na kusudio la pamoja na wakati huo huo kumulika shabaha mpya hasa katika maeneo ambayo vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa vinaendesha operesheni zake katika mazingira magumu.

Hervé Ladsous, amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa pamoja na hayo lakini pia kunahitajika kuchukuliwa kwa hatua za haraka ikiwemo kutoa msaada wa fedha katika maeneo ambayo yanakabiliwa na bajeti ya kiwango cha chini.

Kitendo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na ulinzi wa amani kwa sasa kina jumla ya operesheni 16 zinazofanyika maeneo mbalimbali.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter