Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM yataja majanga kama changamoto kubwa kwa maendeleo kwenye maeneo ya Asia na Pacific

Ripoti ya UM yataja majanga kama changamoto kubwa kwa maendeleo kwenye maeneo ya Asia na Pacific

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo inaonyesha kuwa maeneo ya Asia na Pacific ndiyo yanayoathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo pia yamesababisha athari kwa maendeleo ya kiuchumi ya eneo hilo.

Kulingana na wengi bara la Asia na eneo la Pacific mwaka 2011 utakumbukwa kama mwaka wa majanga makubwa yenye athaari kubwa kwa uchumi , kwa jamii pia kwa maisha ya watu katika eneo hilo. Tetemeko la ardhi lilitokea nchini Japan, gharika ya tsunami ,ajali ya nyuklia pamoja na mafuriko maeneo ya kusini mashariki mwa Asia ni baadhi ya majanga makuu yaliyochangia hasara ya dola 294 eneo hilo ikiwa ni asilimia 80 ya hasara yote duniani kupitia majanga mwaka 2011.