Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zakwamisha oparesheni za UNHCR nchini Lebanon

Ghasia zakwamisha oparesheni za UNHCR nchini Lebanon

Hali ya ukosefu wa usalama pamoja na kuongezeka kwa misukosuko nchini Lebanon vimelazimu shirika la kuhudumia wakimbii la Umoja wa Mataifa UNHCR kusitisha kwa muda uandikishaji wa wakimbizi wa Syria nchini humo.

Kati ya miji ambayo shughuli za uandikishanji zilisimaishwa ni pamoja na mji mkuu Beirut, Tripoli, Akar na Saidia. UNHCR inasema kwamba idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Lebanon imepita wakimbizi 101,000 baada ya wakimbizi 5,500 kuandikishwa juma lililopita. Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa shirika hilo linajaribu kuchunguza hali na lina matumani ya kurejelea oparesheni zake wakati hali itaruhusu.

Kwa sasa hatuna mipango ya kubadlisha jinsi tunavyofaya kazi ndani mwa Lebanon, kumekuwa na usitishaji wa muda wa unadikishaji ambao tunataji utarejelewa hivi karibuni. Kile wakimbizi wanachotuambia ni kuwa hakuna yeyote anayeishi kwenye kambi, wanaishi na jamii ndani mwa Lebanan . Wengi wao wanalaalamikia kuwepo kwa bei za juu. Ni majuma manne tangu tuzindue mpango huu kuhusu Syria na hadi sasa tuna ufadhili wa theluthi tatu.