Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Syria waongezeka, huku Mahitaji ya kibinadam yakipanda

Wakimbizi wa Syria waongezeka, huku Mahitaji ya kibinadam yakipanda

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema idadi ya wakimbizi wa Syria ambao wameandikishwa nchini Lebanon imeongezeka na kuzidi laki moja. Tayari wakimbizi wa Syria wamezidi idadi hiyo ya laki moja katika nchi za Uturuki na Jordan, huku idadi ya wakimbizi wa Syria katika kanda nzima ikiwa imepanda na kuzidi 358, 000. Serikali katika nchi jirani za Syria zinakadiria kuwa kuna maelfu ya wakimbizi wengine wa Syria ambao bado hawajaandikishwa.

Wakati huo huo, mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP katikakanda ya Mashariki ya Kati, Daly Belgasmi, amesema shirika hilo limewafikishia msaada wa chakula wakimbizi wa Syria milioni 1.5, ingawa linapata ugumu kuwafikia kwa sababu za kiusalama.

Nalo Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesema limetoa misaada ya kibinadam kwa familia za wakimbizi wa Iraq ambao wamekimbia kutoka Syria kwa sababu ya hali mbovu ya usalama. Misaada hii sio ya chakula . Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)