Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Colombia iangalie upya mapendekezo ya marekebisho ya katiba: Wataalamu wa UM

Colombia iangalie upya mapendekezo ya marekebisho ya katiba: Wataalamu wa UM

Jopo la wataalamu 11 wa Umoja wa Mataifa limeitaka serikali na bunge la Colombia kuangalia upya mapendekezo ya marekebisho ya katiba hususan sheria za vitendo vya uhalifu unaofanywa na jeshi, kwa kuwa mapendekezo hayo yanaweza kuwa na madhara makubwa katika utawala wa kisheria na utekelezaji wa haki za binadamu nchini humo.

Wito huo umo kwenye barua ya wazi kwa umma iliyotolewa leo na jopo hilo ikionya kuwa endapo mapendekezo hayo yatapitishwa, yatakandamiza utawala wa haki dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo uhalifu unaofanywa na wanajeshi au polisi. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)