Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaandaa mafunzo kwa maafisa wa Iran

IOM yaandaa mafunzo kwa maafisa wa Iran

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, linakusudia kuendesha mafunzo ya siku mbili kwa maafisa wa Iran ikiwajengea uwezo kwenye maeneo ya uhamiaji na maendeleo.

Mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa ushirikiano wa pamoja baina ya IOM na serikali ya Kiislamu ya Iran yamepangwa kufanyika Oktoba 22 na 23 katika jimbo la Mazandaran .

Washiriki kwenye mafunzo hayo yanatazamiwa kupewa mbinu za kisasa zitakazowasaidia kufungamanisha masuala ya uhamiaji na maendeleo.

Washiriki kwenye mafunzo hayo yaliyogharimiwa na serikali ya Japan ni kutoka wizara ya mambo ya ndani, mambo ya nje na maafisa uhamiaj