Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kupunguza vurugu kwenye chaguzi Afrika: UNECA

Hatua zichukuliwe kupunguza vurugu kwenye chaguzi Afrika: UNECA

Katibu Mtendaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa Afrika, UNECA, Carlos Lopes amesema kardi uchumi wa Afrika unavyoimarika, vurugu zitokanazo na chaguzi za kisiasa zitapungua kutokana na kuongezeka kwa uelewa wa raia wake na kutarajia kushiriki zaidi kwenye masuala ya siasa.

Amesema japo chaguzi zimekuwa jambo la kawaida lakini bado uhalali na ubora wake unahojiwa na kupoteza thamani yake na kwamba tofauti kubwa za maendeleo ya kiuchumi katika jamii na ukosefu wa utulivu wa kisiasa vinaweza kusababisha ghasia za kisiasa.