Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kutambua watetezi wa haki za walemavu

Umoja wa Mataifa kutambua watetezi wa haki za walemavu

Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia na Pacific kwa kushirikiana na Jamhuri ya Korea zitatoa tuzo maaluum kwa watu Kumi walio mstari wa mbele kutetea haki za walemavu.

Tuzo hiyo itatolewa tarehe Mosi mwezi ujao huko Incheon, Korea Kusini wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa kuzindua muongo mpya wa harakati za kikanda za kuwa na jamii inayojali na kushirikisha walemavu.

Washindi wa tuzo hiyo waliochaguliwa na jopo la kimataifa ni pamoja na mbunge, kiongozi wa kijamii anayetetea kutokomeza umaskini pamoja na mtetezi wa haki za wanawake. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)