Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICJ yakamilisha kusikiliza malalamiko ya mpaka baina ya Burkina Faso na Niger

Mahakama ya ICJ yakamilisha kusikiliza malalamiko ya mpaka baina ya Burkina Faso na Niger

Burkina Faso na Niger zimekamilisha kuwasilisha malalamiko yao katika mahakama ya kimataifa ya haki juu ya mzozo wa mpaka ambao unagombewa na pande zote. Mahakama hiyo inatazamiwa kutoa maamuzi yake katika kipindi cha miezi minne hadi sita.

Wakati ikiwasilisha madai yake, Burkina Faso ilitaka Mahakama hiyo kuzingatia mpaka ulioasisiwa na koloni la zamani Ufaransa wakati eneo hilo lilijulikana kama Ufaransa ya Afrika Magharibi. Lakini Niger inapinga misingi ya mpako huo ulioasisiwa mwaka 1927 na inataka kuzingatiwa ramani mpya ya mpaka iliyotolewa na taasisi ya jiogrophia ya ufaransa mwaka 1960.

Mahakama hiyo ya kimataifa iliasisiwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1945 kwa ajili ya kusaka suluhu ya kisheria kwa nchi zinazotumbukia kwenye mizozo ya mipaka.