Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumaliza dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo si jambo gumu: Bangura

Kumaliza dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo si jambo gumu: Bangura

Wanaume wakiwemo watoto wa kiume wanazidi kuwa waathiriwa wa dhuluma za kingono kwenye mizozo kwa mujibu wa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo Zainabu Hawa Bangura.

Akiongea mjini Geneva Bi Bangura amesema kulingamiza suala la dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo sio kitu kigumu lakini itahitajika kujitolea kisiasa, kuwepo mabadiliko ya sheria, kuwapa mafunzo polisi na maafisa wamahakama jinsi ya kushughulikia uhalifu huo. Bangura amezishauri serikali kuboresha mifumo yao ya mahakama ili waweze kukabiliana ipasavyo na wanaohusika kwenye vitendo hivi.

Huenda tusijue idadi kamili ya waathiriwa kwa sababu watu huwa wanaona haya kujitokeza kwa kuwa huenda wakanyanyapaliwa na kufukuzwa na jamaii zao au kutishiwa maisha ikiwa watawataja waliowafanyia hivyo. ICC au jamii ya kimataifa hawawachukulii hatua wanajeshi wahusika. Ni lazima tufanye kazi na serikali. Ni lazima tuziruhusu na kuzilazimisha serikali kuchukua usimamizi kwenye suala hili na kutafuta njia za kuhkikisha kuwa kesi hizi zimefikishwa mahakamani . Wacha tuangazia wahusika na sio waathiriwa.”