Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yasema kuna mwelekeo mzuri wa uhusiano na Sudan

Sudan Kusini yasema kuna mwelekeo mzuri wa uhusiano na Sudan

Makubaliano ya hivi karibuni kati ya Sudan na Sudan Kusini yanaonyesha matumaini ya uhusiano mzuri kati ya pande mbili hizo.

Huo ni ujumbe wa balozi wa Sudan Kusini Francis Deng aliowaeleza waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani mara baada ya mkutano na Baraza la Usalama.

Mwezi uliopita Sudan ilitiliana saini makubaliano kadhaa ya ushirikiano na Sudan Kusini ikiwemo katika mafuta, ulinzi na masuala ya uraia. Balozi huyo wa Sudan Kusini amesema kutiwa saini kwa makubaliano hayo ni matokeo ya jumuiya ya kimataifa ikiwemo Baraza la Usalama kushiriki kwa dhati katika mashauriano.

Hata hivyo Balozi Deng amesema hatma juu ya hadhi ya jimbo la Abyei na maeneo mengine yanayogombaniwa na pande mbili hizo bado haijafahamika.

(SAUTI YA BALOZI DENG)