Uzalishaji wa chakula uzingatie uhifadhi wa mazingira: UNEP

16 Oktoba 2012

Ripoti mpya ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP imetaka mjadala wa usalama wa chakula duniani uzingatie masuala ya mazingira ikiwa ni pamoja na kulinda mazingira ya kiekolojia yanayosaidia uzalishaji wa chakula.

Ikiwa imezinduliwa leo wakati wa siku ya chakula duniani, ripoti hiyo iliyoandikwa an wanasayansi na watalaamu 12 imesema kitendo cha kuhifadhi baionuai kitakuwa muhimu katika kulisha wakazi Bilioni Tisa wanaokadiriwa kuwa watakuwa wanaishi duniani mwaka 2050.

James Lomax ni afisa kutoka UNEP.

(SAUTI YA JAMES LOMAX)

"Tunafikia hatua ambayo mifumo yetu ya sasa ya uzalishaji chakula hivi sasa inafanya  ile ya kiasili ishindwe kufanya kazi kuwa tunatumia virutubisho visivyo vya kiasili.”

Ripoti hiyo iliyojikita katika maeneo ya mifumo ya ulaji wa chakula, uzalishaji, uvuvi wa baharini na ufugaji wa samaki, pia imebaini  udhaifu katika mfumo wa usambazaji chakula ambao umesababisha kupotea kwa tani Bilioni Moja na Laki Tatu za chakula kila mwaka.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter