IOM yaanza kuwasambazia misaada ya dharura waathirika wa moto Puntland

16 Oktoba 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, linashirikiana na mamlaka za kikanda nchini Somalia kwa ajili ya kusambaza huduma za dharura kwa familia zaidi 262 ambazo ziko katika hali mbaya baada ya kuathiriwa na moto katika eneo la Gorowe .

Eneo hilo lililoko katika jimbo la Puntland ambalo limeharibiwa na moto limeshuhudia watu wake wakikosa mahitaji muhimu ikiwemo chakula,maji pamoja na sehemu ya kujihifadhi.

IOM ikishirikiana pia na mashirika yasiyokuw aya kiserikali inawasambazia wakazi hao huduma za dharura ikiwemo kupeleka matanki ya maji na huduma nyingine muhimu.

Maafisa katika eneo hilo wamesema kuwa idadi kubwa ya waathirika wa moto huo wanatokea eneo la kusin mwa Somalia. Tangu kuzuka kwa machafuko mwaka 1991 eneo hilo la Punt land limechukua kiasi cha watu 400,000 waliokosa makazi waliokimbia machafuko kutoka kusini mwa Somalia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter