Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mifumo endelevu yahitajika kutokomeza njaa: Ban

Mifumo endelevu yahitajika kutokomeza njaa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake kwa siku ya chakula duniani na kusema kuwa mwelekeo wa pamoja unaochochea vyama vya kilimo vya ushirika ni muhimu katika kufikia lengo la kutokomeza njaa alilozindua wakati wa mkutano wa Rio + 20 nchini Brazil.

Ban amesema kutokomeza njaa ni dira ya kuwa na dunia ambamo mifumo ya chakula ni endelevu na kila mtu anapata haki yake ya chakula na kwamba utaalamu wa hali juu katika vyama hivyo utakuwa muhimu katika kufikia lengo kuu kuongeza maradufu kipato na uzalishaji wa tija kwa wakulima wadogo.