Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yawapatia chakula raia Milioni 1.4 wa Syria

WFP yawapatia chakula raia Milioni 1.4 wa Syria

Zaidi ya raia Milioni 1.4 wa Syria wanategemea msaada wa chakula unaotolewa na Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kutokana na uhaba wa chakula na kupanda maradufu kwa bei ya vyakula katika maeneo yenye mapigano nchini Syria.

Mathalani WFP imesema uhaba wa mafuta umefanya vyakula muhimu kama mikate kutokapatikana kwa sababu viwanda vya kuoka mikate haviwezi kufanya kazi. Bi. Byrs, msemaji wa WFP.

Mgao wa mwezi wa vyakula katika majimbo 14 nchini Syria unafanywa na chama cha mwezi mwekundu nchini humo ambapo WFP imesema ina wasiwasi juu ya hali ya maisha ya wakazi walionasa kwenye maeneo ya mapigano kama vile Homs , Aleppo , Deir Ezzor, Dara na mji mkuu Damascus kwa sababu hawawezi kugawa chakula.