Graziano ataka kujitolea kwa mataifa katika kuangamiza njaa duniani:FAO

15 Oktoba 2012

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO Jose Graziano da Silva amesema kuwa ikiwa mataifa yataweka jitihada zao katika kumaliza njaa lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza kwa nusu idadi ya watu wenye njaa duniani ifikapo mwaka 2015 bado litatimizwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kuhusu usalama wa chakula duniani da Silva amesema kuwa hatua muhimu zimepigwa katika kupunguza idadi ya watu walio na njaa kwa watu milioni 132 tangu mwaka 1990. Ameongeza kuwa bado watu milioni 870 wanatatizwa na njaa wakati mikakati ya kupunguza njaa ikiwa imekwama tangu mwaka 2007. Jason nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter