Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE yahimiza matumizi zaidi ya usafiri wa majini ili kulinda mazingira

UNECE yahimiza matumizi zaidi ya usafiri wa majini ili kulinda mazingira

Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu uchumi barani Ulaya, UNECE, imetoa wito kwa serikali za ulaya kufanya juhudi zaidi ili kuongeza usafiri wa maji, kwani ni njia inayolinda mazingira, ya kutegemewa, salama na gharama nafuu.

Bara la Ulaya lina hadi kilomita 29, 000, za maji yanayoweza kuwa na mikondo ya usafiri, na bandari 400, lakini ni asilimia 7 tu ya bidhaa ndizo zinazosafirishwa kupitia njia ya maji, huku asilimia 78 ya uchukuzi ukiwa barabara kavu asilimia 15 ukiwa kwenye reli.

Shehena nzito nzito zinaweza kusafirishwa kwa konteina, bila kelele, usiku na mchana, kwa mujibu wa UNECE. UNECE imeongeza kuwa usafirishaji kwenye mito Rhine na Danube unaweza kuongezeka kwa hadi asilimia 50 na asilimia 80 mfululizo, bila kuwekeza fedha nyingi zaidi, kwa mujibu wa takwimu za sekta ya uchukuzi. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)