Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia kaskazini mwa Mali yachukua sura mpya: UM

Ghasia kaskazini mwa Mali yachukua sura mpya: UM

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu, Ivan Simonovic amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Mali na kusema kuwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kaskazini mwa nchi hiyo vinaendelea ijapokuwa mwenendo na mazingira yake yamebadilika tangu kuanza kwa mgogoro kwenye eneo hilo.

Ametoa mfano kuwa mwanzoni mwa mgogoro, waasi wa kabila la Tuareg walipokuwa wakiteka maeneo kulikuwepo taarifa za kuuawa kwa askari, ubakaji, wizi na hata watoto kujumuishwa katika majeshi tofauti na sasa. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)