Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 870 wamekuwa wakisumbuliwa na utapiamlo duniani

Watu milioni 870 wamekuwa wakisumbuliwa na utapiamlo duniani

Karibu watu milioni 870 wamekuwa wakisumbuliwa na hali mbaya ya utapia mlo kati ya mwaka 2010 na 2012 kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu njaa iliyotolewa hii leo. Ripoti hiyo yenye kichwa “Hali ya usalama wa chakula duniani mwaka 2012” (SOFI) ilichapishwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo shirika la chakula duniani FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD pamoja na shirika la mpango wa chakula duniani.

Kati ya wanaotaabika, milioni 852 wanaishi kwenye mataifa yanayoendelea karibu asilimia 15 ya watu wote huku asilimia 16 wakiwa wana utapiamlo kwenye mataifa yaliyostawi. Hata hivyo idadi ya watu wanaotaabika na njaa ilipungua kwa watu milioni 132 kati ya mwaka 1990-92 na mwaka 2010-12 au kutoka asilimia 18.6 hadi asilimia 12.5 ya watu wote wote duniani.

(SAUTI YA JOSE GRAZIANO da SILVA)