Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kuna viwango vya ubaguzi visivyokubalika Namibia miaka 20 baada ya uhuru

Bado kuna viwango vya ubaguzi visivyokubalika Namibia miaka 20 baada ya uhuru

Zaidi ya miongo miwili tangu Namibia ilipojipatia uhuru, bado taifa hilo linaendelea kuzingirwa na viwango visivyokubalika vya kutokuwepo usawa kwenye misingi ya jinsia, kabila, kikanda pamoja na tabaka, ameonya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini uliopindukia na haki za binadamu, Magdalena Sepulveda.

Akiongea baada ya kukamilisha ziara yake nchini Namibia Sepulveda amesema kuwa anatambua uharibifu uliofanywa na wakoloni lakini hata maendeleo hayaja kuwa kwa mwendo unaotakikana, akiongeza kuwa Namibia ni taifa ambalo limeshuhudia uthabiti na ukuaji wa uchumi tangu lipate uhuru. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)