Tunachoomba ni huruma, asema mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel

8 Oktoba 2012

Naye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu, Tawakkol Karman, ameanzisha mbiu ya huruma kwa ajili ya Syria wakati wa kongamano hilo la demokrasia mjini Strasbourg, Ufaransa. Bi Karman ambaye ni mwandishi wa habari kutoka Yemen ameelezea pia kuvunjwa moyo na mateso wanayopitia wanadamu.

Akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo, mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ametoa wito wa msaada kwa watu wa Syria, na kutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua pale ukiukaji wa haki unapopatikana.

Amesema demokrasia na maendeleo ni vitu vinavyokwenda sambamba, na kwamba matumaini ya mkutano wa Rio mwaka 1992 yalikuwa hayajafikiwa, kwani uongozi wa kiimla na ufisadi bado umeenea, na hivyo kuacha malengo ya maendeleo nyuma.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud