UM wataka marekebisho katika sekta ya benki ili kulinda haki za binadam

5 Oktoba 2012

Kundi la wataalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini ulokithiri, madeni ya kitaifa na utaratibu wa usawa, limezikumbusha serikali za Muungano wa Ulaya kwamba marekebisho ya kiuchumi ni lazima yaende sambamba na wajibu wa serikali wa kulinda haki za binadamu. Hii ni kufuatia ripoti ya utafiti uliofanywa kuhusu sekta ya benki katika mataifa yote ya Muungano wa Ulaya, EU.

Wakirejelea ripoti ya Liikanen, ambayo inapendekeza baadhi ya hatua za utaratibu unaotakiwa ili kuwalinda walipa ushuru kutokana na mzigo wa kuokoa kampuni zinazofilisika na kuufanya mfumo wa fedha kuyumbayumba,wataalam hao wametoa wito kwa serikali za EU zihakikishe kuwa fedha muhimu za umma hazitumiki kuzisaidia taasisi za fedha ambazo zinafilisika katika siku zijazo.

Wamesema serikali zina wajibu wa kuchukua hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha haki za umma zimeheshimiwa na kulindwa, zikiwemo kuhakikisha kuna rasilmali za kutosha kuwasaidia watu wanaoishi katika umaskini wa kupindukia. Joshua Mmali na taairfa kamili.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud