Walimu milioni 1.7 wanahitajika ili kufikia lengo la milenia kuhusu elimu: UM

5 Oktoba 2012

Walimu milioni 1.7 zaidi wanahitajika ili kuwezesha kufikia lengo la milenia la elimu ya msingi kwa wote ifikapo mwaka 2015. Hayo ni kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, katika kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani leo Oktoba 5.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Irina Bokova, ametoa wito kwa serikali ziweke mazingira yanayofaa kikazi, mafunzo ya kutosha kitaaluma na mifumo ya kulinda haki za walimu, pamoja na mishahara inayoenda sambamba na umuhimu wa taaluma ya ualimu.

(SAUTI YA IRINA BOKOVA)

Mshairi maarufu, William Butler Yeats aliwahi kulinganisha elimu na kuwasha moto. Walimu ndio miyale mikubwa zaidi. Kila mmoja wetu anakumbuka mwalimu wetu tuliyempenda zaidi, na hisia za ajabu na hamu ya kutaka kujua walizoibua ndani yetu. Ndiyo maana leo, ni lazima sote tuwe na msimamo kwa ajili ya walimu

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani, ILO, Guy Ryder, amesema walimu wengi wanaikimbia taaluma ya ualimu kwa sababu ya hadhi iloshuka kutokana na mishahara midogo na mazingira yasiyotoa hamu kwa watu kujiunga nayo. Amesisitiza umuhimu wa elimu katika harakati za kuweka maendeleo endelevu, na kuelezea heshima yake kwa walimu

(SAUTI YA GUY RIDER)

"Elimu ni mojawepo ya misingi tisa ya maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii. Kwa hivyo, kila dola inayowekezwa vyema katika elimu, inajenga nafasi za kazi, uzalishaji zaidi na jamii imara zaidi. Watoto walio shuleni wana nafasi nzuri ya kuepukana na mzigo wa ajira ya watoto. Kwenye siku ya walimu duniani, tunatoa heshima zetu kwa wanawake na wanaume ambao hutoa mafunzo kwa wanafunzi kote duniani. Walimu na wahadhiri wana jukumu la kutoa ujuzi na maarifa, pamoja na maadili ambayo ni muhimu kwa kuwa na jamii imara."

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania alielezea vitu vinavyohitajika ili kutoa elimu bora, yakiwemo mafunzo ya walimu

(SAUTI YA RAIS KIKWETE)