Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani Syria kufuatia shambulizi la mji wa Uturuki

Baraza la Usalama lalaani Syria kufuatia shambulizi la mji wa Uturuki

Baraza la Usalama limelaani vikali shambulizi la makombora lililofanywa na wanajeshi wa Syria kwenye mji wa Akcakale, na ambalo liliwaua watu watano na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Zaidi ya watu 18, 000, hususan raia, wameuawa nchini Syria tangu migogoro baina ya serikali ya rais Bashar al-Assad na makundi ya upinzani ilipoanza, huku wengine milioni 2.5 wakiwa wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Katika taarifa ya pamoja, wanachama wa Baraza la Usalama limesema tukio hilo limedhihirisha ukubwa wa athari za mzozo wa Syria nchi jirani zake na kwa amani na utulivu wa eneo zima. Wametaka vitendo kama hivyo vya kukiuka sheria za kimataifa vikomeshwe mara moja, na kwamba visirudiwe tena. Wametoa wito kwa serikali ya Syria iheshimu uhuru na mipaka ya jirani zake. Balozi Gert Rosenthal wa Guatemala, ambaye ndiye rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Oktoba, aliwasilisha ujumbe wa Baraza hilo.

(SAUTI YA BALOZI ROSENTHAL)