Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuchunguza biashara inavyoathiri haki za binadamu Mongolia

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuchunguza biashara inavyoathiri haki za binadamu Mongolia

Kundi la wataalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na haki za binadamu, watafanya ziara nchini Mongolia kati ya Oktoba 8 na 18, ili kuchunguza athari za shughuli za biashara dhidi ya haki za binadam nchini humo.

Mmoja wa wataalam hao, Margaret Jungk, amesema Mongolia ni mojawapo wa uchumi unaokuwa kwa viwango vya haraka zaidi duniani, na unatarajiwa kuendelea kukua kwa viwango hivyo katika karne moja ijayo. Hata hivyo, amesema viwango hivi vya ajabu vya ukuaji vinavyotokana na viwango vya juu vya biashara, huenda vikawa na dosari ya athari za ajabu dhidi haki za binadam za wale wanaoishi nchini humo.

Baraza la Haki za Binadam la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kanuni mpya kuhusu uhusiano kati ya biashara na haki za binadam mnamo mwaka wa 2011, mwongozo ambazo kwa mara ya kwanza ziliweka mwongozo wa kimataifa wa kukabiliana na athari mbaya za shughuli za biashara kwa haki za binadam. Uchunguzi wa wataalam hao huru nchini Mongolia ndio utakuwa wa kwanza wa aina yake kufanywa kwa kufuata kanuni hizo, tangu zilipowekwa.