Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandamano ya wapenzi wa jinsia moja yaruhisiwe: Pillay

Maandamano ya wapenzi wa jinsia moja yaruhisiwe: Pillay

Kamishna wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya Serbia ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara iliyopangwa kufanyika Jumamosi na badala yake ameitaka serikali hiyo kufanikisha mikutano hiyo ikiwemo ule wa kujitambua wa wapenzi wa jinsia moja na watu waliobadili jinsi zao ili waweze kutekeleza haki yao ya msingi ya kujumuika pamoja kwa amani na na kujieleza.

Kauli ya Pillay imekuja baada ya taarifa ya wizara ya mambo ya Ndani ya Serbia kupiga marufuku mikutano yote ya Jumamosi kwa madai ya hali ya usalama, sababu ambazo pia zilitumiwa mwaka jana kupiga marufuku mikutano kama hiyo. Mwaka 2010, maandamano ya kujitambua ya watu wanaofanya mapenzi kwa jinsia moja yaliyofanyika Belgrage yalikumbwa na visa kadhaa ikiwemo waandamanaji kushambuliwa kwa mawe, uporaji na hata polisi na watu wengine kujeruhiwa. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(SAUTI YA ASSUMPTA MASSOI)