Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya walinda amani wa UNAMID

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya walinda amani wa UNAMID

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mauaji ya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Darfur, UNAMID, ambayo yalitekelezwa tarehe mbili Oktoba jioni na watu wasojulikana. Wanajeshi wanne waliuawa katika shambulizi hilo dhidi ya askari walinda doria kutoka Nigeria katika eneo la El Geneina magharibi mwa Darfur, huku wengine wanane wakijeruhiwa.

Wanachama wa Baraza la Usalama wametoa wito kwa serikali ya Sudan kufanya uchunguzi haraka na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.

Wameongeza kuendelea kuunga mkono kwa dhati ujumbe wa UNAMID, na kutoa wito kwa makundi yote kwenye jimbo la Darfur kushirikiana na nao.

(SAUTI YA ROSENTHAL)