Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira kwa vijana bado ni tatizo kwenye mataifa ya G20:ILO

Ajira kwa vijana bado ni tatizo kwenye mataifa ya G20:ILO

Shirika la kazi duniani ILO limesema kuwa ajira kwa vijana linabaki kuwa changamoto kuu wakati vijana milioni 17.7 wakiwa hawana ajira au zaidi ya asilimia 16 kwenye nchi 17 kati ya nchi zilizostawi na zinazoinukia kiuchumi za G20 wakiwa hawana kazi.

Kulingana na takwimu zilizowasilishwa kwenye mkutano wa kundi la nchi za G20 mjini Geneva zinaonyesha kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana unazidi kupanda ukiwa ni kati ya asilimia 8 na hadi 50 kwenye nchi 17 kati ya nchi 20 wanachama. Kwa muda wa miezi 12 iliyopita ukosefu wa ajira kwa vijana uliongezeka kwa silimia 10 huku idadi ya watu wanaofanya kazi ikipungua kwenye nchi 12. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)