Sisi ndiyo wenye uwezo wa kuupa nguvu UM

2 Oktoba 2012

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremic, amezungumzia kile alichokiita nguvu za Umoja wa Mataifa akisema kuwa zitadhihirika iwapo tu nchi wanachama zitaamua hivyo

Akizungumza wakati wa kufunga mjadala uliowahusisha maafisa wa ngazi za juu, rais Vuk alizitolea mwito nchi wanachama kufanya kazi kwa pamoja ili kuupa nguvu Umoja huo wa Mataifa.

Aliwataka watendaji wenzake kuamka na kuanzisha shabaha ambayo itaamusha hali ya uwazi na uwajibikaji kuhusiana na utendaji wa chombo hicho cha kimataifa.

Alisema kuwa lile linalopaswa kufanyika sasa lisingoje kesho na akataka kujenga hali ya kuaminiana miongoni mwa nchi wanachama.